COVID-19 UPDATES
Shukrani kwa Mungu, baada ya kukaa nyumbani miezi miwili kutokana na janga la Corona, tuna furaha kufungua chuo leo tarehe 1st June 2020 na tunafuraha pia wanafunzi wote waliorepoti leo wakiwa wazima wa afya.
Sisi kama taasisi tunaendelea kufuata taratibu zote zilizowekwa na wizara ya Afya ili kujikinga na maambukizi ya COVID-19. Kwahiyo tunawaomba wafanyakazi wote, wageni pamoja na wanafunzi waendelee kufuata utaratibu mzuri uliowekwa ili kujikinga na maambukizi hayo hatari ya Korona.
TAHADHARI ZA KUZINGATIA
-
Hakikisha unanawa mikono yako kwa maji tiririka kila wakati hasa wakati wa kuingia getini.
-
Kaa umbali wa angalau mita 1 (miguu 3) kati yako na wengine. Kwa nini? Wakati mtu akikohoa, kupiga chafya, au kuongea hutoa majimaji kutoka kwenye pua au mdomo ambao unaweza kuwa na virusi. Ikiwa uko karibu sana, unaweza ku[pata virusi vya COVID-19 ikiwa mtu huyo ana ugonjwa.
-
Epuka kukaa sehemu zenye mikusanyiko wa watu. Kwa nini? Mahali watu wanapokutana kwa umati, una uwezekano mkubwa wa kuwasiliana karibu na mtu ambaye ana COIVD-19 na ni ngumu zaidi kudumisha umbali wa mita 1
-
Epuka kugusa macho, pua na mdomo. Kwa nini? Mikono inagusa vitu vingi na inaweza kuchukua virusi. Mara baada ya kuchafuliwa, mikono inaweza kuhamisha virusi kwa macho yako, pua au mdomo. Kutoka hapo, virusi vinaweza kuingia mwili wako na kukuambukiza.
-
Hakikisha wewe, na watu wanaokuzunguka mnafuata usafi mzuri wa kupumua. Hii inamaanisha kufunika mdomo wako na pua kwa kiwiko cha mkono wako au tishu wakati unapokohoa au kupiga chafya. Kisha tupa tishu zilizotumiwa mara moja na osha mikono yako.
Note: Tafadhari wasiliana nasi kupata maelezo zaidi.
Brother Msofe : 0755651360
Principal Tech - Fr. Bonifas mchami : 0756308518
Mapokezi – Mr. Ikaku : 0759005337
Baruapepe: secretary@donboscododoma.org
Tovuti : www.donboscododoma.org